Dalili za Kiwewe

Hii ni orodha ya dalili maarufu ambazo watu huwa nazo baada ya kiwewe. Hii inaweza kuwa muhimu unapoelezea watoto (au watunzaji wao) jinsi kile wanachohisi (kimwili, kihisia, kiakili) kinahusiana na walichopitia. Watu wengi wanaamini kuwa ni wao pekee wanaohisi jinsi wanavyohisi. Inaweza kusaidia kujua kuwa hawako peke yao na dalili zao ni “hisia za kawaida kwa hali zisizo za kawaida.”


Baadhi ya dalili maarufu za mwili zinaweza kuwa

  • Kusaga meno
  • Tatizo la tumbo, kichefuchefu
  • Maumivu ya kichwa
  • Mashambulizi ya wasiwasi
  • Kushindwa kujizuia kukojoa/kukojoa kitandani kwa muda mrefu
  • Hali ya kutotuliaama

Baadhi ya dalili maarufu za kisaikolojia zinaweza kuwa

  • Huzuni na kulia sana
  • Msukosuko au “kuhisi kujidhuru” mara kwa mara
  • Tabia ya vurugu na upinzani
  • Kupoteza hamu ya kucheza
  • Hamu za kuchukua tahadhari zaidi, kushiriki kwenye tabia hatari
  • Tabia za kulazimisha
  • Matatizo ya uhusiano (Mifano: Kujitenga au woga wa kutangamana) Kukasirishwa haraka – kuwakaripia watu “bila sababu”
  • Kujiondoa
  • Wasiwasi
  • Kukosa uwezo wa kuondoa “picha akilini mwangu”
  • Tatizo la kuenda kwenye eneo la ajali au tukio la kiwewe – kutotaka kurudi
  • Kuwazia tukio la kiwewe – kufikiria na/au kuzungumzia kiwewe wakati wote Kurejelea yaliyopita au kumbukumbu za kudukiza, haswa ikiwa kitu kinachohusiana na tukio kinarudiwa (mtu akivaa mavazi yaleyale kama mwathiriwa, harufu iliyokuwepo kwenye tukio, kelele zilezile – kama vile ving`ora, taa zinawaka na kuzimika ghafla, n.k.)
  • Kuanza woga kwa ghafla
  • Kutaka kulala wakati WOTE
  • Mabadiliko ya hamu ya chakula – kutohisi njaa hadi kula zaidi

Haswa kwa watoto, huenda kukawa woga wa

  • Kutengana, kukataa kutenganishwa na watunzaji watu wazima
  • Kulala kwenye chumba chake cha kulala au matatizo ya kulala (hofu za usiku, majinamizi)
  • Kuenda kwa yaya, kwenye kituo cha malezi ya kutwa, shule au kanisa
  • Kuwa na mtu maalum
  • Giza (zaidi na juu ya, au mabadiliko kutoka woga wa giza wa mtoto wa “kawaida” au wa kawaida wa ukuaji)
  • Vifaa fulani (ambavyo hakuwa akiviogopa awali)
  • Kuenda kwenye bafu

Watoto wachanga wanaweza kuwa na tabia za kurudi nyuma kama vile

  • Kukosa kuwa imara
  • Kunyonya kidole gumba
  • Kupoteza hatua za ukuaji, kama vile mafunzo ya kutumia poti au kurudi nyuma kwa lugha

Watoto walio na umri wa kuenda shuleni wanaweza

  • Kuwa na matatizo ya kusoma
  • Kuacha kuhudhuria madarasa, kutoenda shuleni
  • Kuwa na matatizo ya kumakinika, alama za kufeli
  • Kuunda michezo au mchoro unaosawiri vurugu