1. ForChildren.com ni nini?

ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano kusaidia kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio hatarini. Sisi ni jamii ya duniani kwote ya wafuasi wa Yesu iliyojitolea kwa ukuaji wa watoto wa jumla. Jiunge na seminari, madhehbu ya kanisa, mashiriki yasiyo ya faida, makanisa na watu binafsi walioungana KWA NIABA YA WATOTO.

 

2. Kwa nini Compassion International ilitengeneza tovuti hii?

Hadi 2015, Compassion International inahudumia watoto milioni 1.7 wanaoishi katika umaskini; hata hivyo, kuna zaidi ya watoto milioni 400 wanaoishi katika umaskini. Na hao wengine? Ingawa changamoto ni kubwa kuliko Compassion, sio kubwa kuliko Kanisa. Kwa kutengeneza ForChildren.com, Compassion inatoa ujuzi, vifaa na tajirbi kutoka kwa zaidi ya miaka sitini ya ukuaji wa jumla wa mtoto, na huunda eneo la watu wengine kufanya hivyo. Pamoja tunatumiani kulisaidia Kanisa kuwaachilia watoto WOTE kutoka kwa umaskini na wawape nidhamu kamili ya kutimiza uwezo wao kamili.

 

3. Nani anaweza kutumia rasilimali za ForChildren.com?

Mtu yoyote! Hii ni jamii inayoshirikiana ya kushiriki rasilimali na mawazo. Ili maudhui yachapishwe na yaweze kufikiwa, lazima yatimize vifezo fulani. Bofya hapa ili uone miongozo ya uwasilishaji.

 

4. Ninawasilishaje rasilimali?

Kutoka kwa ukurasa wa nyumbani wa ForChildren.com, bofya Discover. Juu ya ukurasa, kuna kitufe kinachosema "Shiriki Rasilimali." Bofya kitufe hicho, na ukamilishe fomu ya uwasilishaji. Ukishamaliza, vofya Wasilisha! Kuwasilisha rasilimali kunaituma kwa afisa mwangalizi atakayeipitia na kuhakikisha inatimiza Miongozo ya Uwasilishaji ya ForChildren.com kabla ya ichapishwe kwenye tovuti.

 

5. Niliwasilisha rasilimali, lakini siioni kwenye tovuti. Ni nini kilifanyika?

Baada ya kuwasilisha rasilimali hiyo, mkaguzi huipitia kuhakikisha inatimiza Miongozo ya Uwasilishaji ya ForChildren.com.  Baada ya kuiwasilisha, utapokea barua pepe ya uthibitishaji kwamba rasilimali imewasilishwa; pia utajulishwa wakati hali itabadilika kutoka "Inasubiri" na kuwa "Imeidhibishwa" au "Imekataliwa". Ikiwa "Imekataliwa", kutakuwa na maelekezo kuhusu jinsi ya kutatua tatizo na kuwasilisha upya. Baada ya kupokea notisi kwamba rasilimali "Imeidhinishwa," itaweza kufikiwa kupitia kipengele cha Discover kwenye ForChildren.com.

6. Ninawasilishaje rasilimali nyingi zinazohusiana?

Ikiwa una rasilimali nyingi zinazohusiana kwenye seti, unaweza kuziwasilisha kama mfululizo. Kwenye ukurasa wa Discover, bofya kitufe cha "Shiriki Mfululizo." Kamilisha fomu ya uwasilishaji wa Mfululizo, na ubofye "Wasilisha." Kisha utaelekezwa kwenye ukurasa wa Mfululizo unapoweza kupakia kila rasilimali iliyo mojawapo wa mfululizo, moja kwa moja.

 

7.  Ninaanzaje Majadiliano ya Muunganisho?

Kwenye kwa ukurasa wa nyumbani wa ForChildren.com, bofya Discover. Ukurasa wa Muunganisho una orodha ya majadiliano yote yanayoendelea; unaweza ktuafuta na kuona kama kuna mtu ambaye tayari amekuwa akiznugmza kuhusu mada yako, au unaweza kubofya kitufe kinachosema "Anza Majadiliano" ili unazishe moja!

 

8. Ninatazama maelezo yangu mafupi wapi?

Baada ya kuingia, angalia kwenye ukurasa wa mwanzi wa ForChildren.com kwa viungo vitatu vyenye rangi ya samawati fifu upande wa juu kulia; kiungo kimoja kitakuwa jina lako. Ukibofya kwenye kiungo hicho, kitakupeleka kwenye ukurasa wa maelezo yako mafupi, mahali unapoweza kudhibiti uwasilishaji wako, uendelee kufuata majadiliano unayoshiriki, upakie picha ya maelezo mafupi, ubadilishe nenosiri lako, utazame maktaba zako, na mambo zaidi!

 

9. Nimesahau nenosiri langu. Nifanye nini?

Kwenye ukurasa wa ingia, chini ya sehemu za jina la mtumiaji na nenosiri, bofya kiungo cha rangi ya samawati kinachosema "Umesahau nenosiri lako?" Kitakupeleka kwenye ukurasa unapoweza kuingiza anwani yako ya barua pepe. Tutakutumia barua pepe iliyo na kiungo kitakacho kuruhusu ubadilishe nenosiri lako. 

 

10.  Ikiwa ninahitaji msaa au nina maswali ambayo hayajajibiwa, nifanye nini?

Upande wa chini kulia wa ukurasa wa mwanzo wa ForChildren.com, bofya kiungo cha rangi ya kijivu kinachosema "Wasiliana". Unaweza kuwasilisha ujumbe kwenye timu ya ForChildren, na tutawasiliana na wewe baada ya muda mfupi!