Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Kategoria | Kimwili |
Copyright Owner | Compassion International |
Kitengo hiki kimetayarishwa watoto wa kati ya miaka 3-5. Kinahusisha masomo arobaini na nne, yatakayosaidia kumjenga mtoto kimwili. Masomo yatahusisha mada kama: watu wenye tofauti maalumu, kuisaidia familia, kulisaidia kanisa, Mungu anataka niitunze dunia, Mungu anataka nijitunze. Kila mojawapo ya masomo haya arobaini na nne yanahusisha, mpangilio wa somo (Urefu,matayarisho na vifaa vya kutumia). Muda wa darasa, unaohusisha maelezo kwa kina, jinsi ya kufunza, pamoja na michezo na shughuli zinazowashirikisha wanafunzi ili kuwasaidia kusoma na kuelewa. Kuna tathmini ya mwalimu na ya mwanafunzi pia. Masomo na shughuli za utendaji zinadhamiriwa kutumiwa kwa makundi.
ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio katika mazingira hatarishi. Sisi ni jamii ya wafuasi wa Yesu duniani kote iliyojitolea kwa ajili ya ukuaji wa watoto kiujumla. Tunakualika ujiunge nasi katika jamii hii yenye ushirikiano ili kushirikisha mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika changamoto.
ForChildren.com inatolewa na Compassion International, shirika lisilo la faidia lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.