Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
| Kategoria | Kanisa Filosofia |
| Copyright Owner and Year | Compassion International, 2023 |
Kanisa ndio tumaini kubwa kwa dunia, chombo cha Mungu cha kuendeleza ufalme wake. Compassion International ni shirika lisilo la faida linalojaribu kuunganisha na kuhamasisha Kanisa la dunia kutimiza jukumu lake la ufuasi wa jumla kwa watoto walio katika umaskini. Ikiwa na uzoefu wa miaka sitini ya kutekeleza ukuaji wa jumla kupitia kanisa la ndani, Compassion imetengeneza uelewaji msingi wa Kanisa na jinsi lina jukumu muhimu katika vita dhidi ya umaskini, na vilevile ulinzi na ukuaji wa watoto walio hatarini. Kijitabu hiki, kinachotolewa kwa mara ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili, kinafafanua falsafa ya Compassion kuhusu Kanisa. Kanisa ni nini? Kwa nini Kanisa ni muhimu? Kanisa linafaa kuwa na jukumu gani katika umalizaji wa umaskini na ukuaji wa watoto duniani?
ForChildren.com inatolewa na Compassion International, shirika lisilo la faidia lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.