Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Kategoria | None |
Copyright Owner | Chrissy Sykes |
Hati ya Mpango Kamili wa Mwili Wangu ni Mwili Wangu inatoa njia rahisi, ya hatua kwa hatua ya kujadili na watoto mada nyeti au ambayo huenda hutaki kujadali ya kuzuia unyanyasaji wa watoto. Kuna mashauri ya kuwajulisha watoto wadogo kuhusu mada hizi kwa kuzingatia umri wao ama kwa njia inayofaa kwa umri wao, pamoja na mambo ya kujadili na vifaa vya ziada vya kukusaidia kuwaongoza watoto kupitia video za muziki za Mwili Wangu ni Mwili Wangu. Kuna orodha ya “Maswali Yananayoulizwa Mara Nyingi” ya kukusaidia ujiandae kwa mambo ambayo huenda watoto wakuulize unapowasilisha mada hii na mawazo ya jinsi unavyoweza kujibu maswali hayo. Katika Hati ya kufundisha ya Mwili Wangu ni Mwili Wangu, utapata pia maelezo ya na viashirio vya aina tofauti za unyanyasaji, pamoja na mashauri ya unachoweza kufanya ukishuku kwamba mtoto ananyanyaswa.
ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio katika mazingira hatarishi. Sisi ni jamii ya wafuasi wa Yesu duniani kote iliyojitolea kwa ajili ya ukuaji wa watoto kiujumla. Tunakualika ujiunge nasi katika jamii hii yenye ushirikiano ili kushirikisha mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika changamoto.
ForChildren.com inatolewa na Compassion International, shirika lisilo la faidia lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.