Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Kategoria | None |
Copyright Owner | Chrissy Sykes |
Mwili Wangu ni Mwili Wangu ni mpango wa bure wa kuzuia unyanyasaji wa watoto unaowawezesha ama kuwaelimisha watoto kupitia burudani, video za muziki za katuni. Mpango huu unakusudiwa kuwasaidia watunzaji na watoto wazungumze, huku pia ukiweka mazingira salama ambapo watoto wanajua kwamba wanaweza na wanapaswa kumueleza mtu mzima anayejali ikiwa kuna shida. Video tano za katuni zenye nyimbo zinawasaidia watoto kuwa na hisia njema kuhusu miili yao, pamoja na kuweza kujidhibiti na kuwa na ujasiri kwa kuwapea ujuzi wa kuzungumza wanapokuwa na wasiwasi sana. Muziki na video za katuni zinawakumbusha watoto ujumbe muhimu, nzuri ama unaofaa kwenye Mwili Wangu ni Mwili Wangu. Pata taarifa na vifaa vya ziada kwenye www.mybodyismybody.com/swahili-website-mwili-wangu.
ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio katika mazingira hatarishi. Sisi ni jamii ya wafuasi wa Yesu duniani kote iliyojitolea kwa ajili ya ukuaji wa watoto kiujumla. Tunakualika ujiunge nasi katika jamii hii yenye ushirikiano ili kushirikisha mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika changamoto.
ForChildren.com inatolewa na Compassion International, shirika lisilo la faidia lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.