Sisi ni wafuasi wa Yesu. Tunaamini kwamba watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu zinazofaa kutunzwa, kulindwa, na kulewa. Cha kusikitisha ni kwamba mamilioni ya watoto hao wanateseka na wako hatarini. Kuna zaidi ya watoto milioni 400 wanaoishi katika umaskini mkubwa duniani kwote.[1] Yesu hakutuamuru tuwachunge maskini na walio hatarini peke yake bali pia alitufunza kwamba watoto wanafaa kujumuishwa, kulindwa, na kupendwa. Alikuwa upande wa watoto, na kwa hivyo pia sisi.
Tunaamini kwamba ustawi wa jamii wa siku za baadaye, jumuiya, familia na makanisa unategemea ukuaji wa jumla wa watoto leo. Kwa hivyo, tuko hapa kuimarisha uwezo wa makanisa ya ndani kutoa uchungaji fanisi wa ukuaji wa watoto wa jumla kwa watoto - hasa walio katika umaskini.
ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, inajaribu kuunda jamii ya wafuasi wa Yesu waliojitolea kuwatoa watoto kutoka umaskini, jamii ya waumini wanaoishi wakiwa tayari kusaidia; jamii inayoshiriki ujuzi, mbinu, uzoefu na mawazo ambayo kila mmoja wetu ako nayo kusaidia katika uchungaji wa watoto walio hatarini.
Tunakualika ujiunge nasi katika jamii yenye ushirikiano kushiriki mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika shida.
[1] Olinto, P., Beegle, K., Sobrado, C., & Uematsu, H. (2013). Hali ya Watu Maskini: Maskini Wako Wapi, Ni Wapi Pagumu Zaidi Kumaliza Umaskini, na Wasifu wa Sasa wa Maskini Duniani Ukoje? Kigezo cha Uchumi, 125. doi:Oktoba 2013